SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Mwenyekiti wa Baraza, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Abdulrahman AL-SUMAIT, kwa niaba ya Wanajumuiya wote wa SUMAIT, anatoa salamu za pole kwa Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan, Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, familia, ndugu, jamaa na Watanzania wote kwa ujumla kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Daima tutakumbuka, kuuenzi na kuuthamini mchango wake mkubwa katika ujenzi wa Taifa letu.

Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani Marehemu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

SISI NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA.

Leave a Reply